Michezo

Manchester City kuanza usajili wake wa kwanza kwa kiungo wa Napoli ya Italia

Mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza Manchester City wanatarajia kukamilisha usajili wake wa kwanza msimu huu kwa kuingia mkataba na kiungo wa kati wa klabu ya Napoli ya nchini Itali, Jorge Luiz Frello Filho maarufu kama Jorginho kwa dau la pauni milioni 46.5.

City ambayo haijaingia kandarasi na mchezaji yeyote toka dirisha la usajili kufunguliwa inatarajia kumsaini, Jorginho mwenye uraia wa nchi mbili Brazil na Italia mwishoni mwa wiki hii.

Napoli wanatarajia kutangaza mbadala wa Jorginho mara baada ya mchezaji huyo kuhamia City rasmi  dili ambalo linatarajiwa kukamilika wikiendi hii.

City pia inahitaji kumsajili Riyad Mahrez kutoka kwenye klabu ya Leicester lakini bado ipo kwenye mazungumzo na timu hiyo juu ya dau la pauni milioni 65 linalo hitajika kwa kiungo huyo mshambuliaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents