Burudani

Bendi ya Hifadhi ya Ngorongoro yatangaza deal kwa waimbaji

Msanii wa muziki wa asili ambaye pia ni Balozi wa Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Mrisho Mpoto ametangaza deal kwa waimbaji pamoja na wapiga ala za muziki kujitokeza kwa wingi Sabasaba jijini Dar es salaam katika banda la maonyesho la Hifadhi ya Ngorongoro kwaajili ya kupata wasanii wapya watakao unda bendi mpya ya hifadhi hiyo.

Mrisho Mpoto akiwa na vazi la Tembo

Akiongea wa wadau waliojitokeza kwa wingi katika banda hilo, Mrisho Mpoto ambaye ni balozi wa hifadhi hiyo, alisema vijana hao wanatakiwa kujua kuimba pamoja na mambo mbalimbali yanayohusu Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na vitu vinavyopatikana.

“Hii fursa kwa waimbaji wa muziki pamoja na wapiga ala za muziki, tunatakiwa kuanzisha bendi ya muziki ‘Ngorongoro Band’, kuandaa nyimbo maalum ambazo zitakuwa zinawaelimisha watanzania juu ya ufahari wa hifadhi hii. Kuandaa wimbo ambazo zitawafanya watanzania kuijua zaidi mbuga zao , masuala ya utalii pamoja na vitu mbalimbali vilivyomo ndani yake,” alisema Mpoto.

Naibu Muhifadhi wa Ngorongoro, Asangue Bangu (aliyeshika mic) akieleza jambo akiwa katika banda balozi wa Ngorongoro, Mrisho Mpoto.

Katika hatua nyingine Mrisho amesema anawashukuru wadau mbalimbali wanaojitokeza kwa wingi katika banda la Ngorongoro kwaajili ya kujifunza mambo mbalimbali kuhusu hifadhi hiyo pamoja na wanyama wanaopatika.

“Kusema kweli mambo yamekuwa mazuri sana katika banda letu, watu wanakuja kwa wingi sana kwa sababu sisi tunatoa burudani na elimu, burudani na elimu, kuna bendi hapa In African ambayo inatoa burudani kila siku, kuna mastaa mbalimbali wanakuja kutoa burudani kama mlivyowaona akina Stara Thomas, Solid Ground, Steve B&B na wengine wengi ambao wanakuja na kuondoka. Kwa hiyo kikubwa zaidi kwetu ni burudani na elimu na kusema kweli wengi wamelielewa somo,” alisema Mpoto.

Aliongeza, “Pia tumekuwa na kipengele cha elimu kuhusu wanyama kila siku na baada ya hapo tunawaita watoto waeleze vitu ambavyo wamejifunza kila siku na tumekuwa tukitoa zawadi ya mpaka tsh milioni moja kwa siku na tumeona matunda kabisa watoto wanakuja hapa hawajuhi chochote lakini wakiondoka hapa wanaweza kueleza vitu mbalimbali ambavyo vinapatika katika hifadhi ya Ngorongoro,”

Mshairi huyo amewataka watanzania kwa ujumla kutembelea banda hilo pamoja na watoto wao ili wapate kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Hifadhi ya Ngorongoro.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents