Burudani

Bobbi Kristina kuzikwa Jumatatu ijayo pembeni mwa kaburi la mama yake marehemu Whitney Houston

Familia ya marehemu Bobbi Kristina – mtoto wa Bobby Brown na marehemu Whitney Houston, itakusanyika Jumamosi hii August 1 kuomboleza na kusheherekea maisha ya mpendwa wao aliyefariki dunia Jumapili iliyopita, ikiwa ni miezi sita toka alipodondoka bafuni na kupoteza fahamu.

bobbi n whitney

Kwa mujibu wa US Magazine, ndugu watakusanyika katika kanisa la St. James United Methodist huko Alpharetta, Georgia, Marekani Jumamosi, na atazikwa Jumatatu ijayo August 3 pembeni mwa alipozikwa marehemu mama yake Whitney Houston, katika makaburi ya Fairview huko New Jersey.

Chanzo kimoja kimesema kuwa hapo awali ndugu akiwemo baba yake Bobbi, Bobby Brown walipanga kukusanyika Alhamisi hii kufanya maombolezo, lakini walibadili na kusogeza hadi Jumamosi ili kuwapa nafasi wapendwa wake wote kuhudhuria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents