Makala

#Bongo5hamasa. Umefeli, umeachwa ? usikate tamaa kesho yako ni nzuri zaidi

Hebu tupeane moyo asububi asubuhi ile tuwe na moyo wa kupambana katika harakati zetu 😂. Chukua hii:- kwa kuanza na nukuu ya jack ma ,mwanzilishi wa alibaba na tajiri namba 22 duniani kwa mujibu wa Forbes

Anasema “Nilifeli mara 3 chuoni. Nilituma maombi ya kazi mara 30 lakini mara zote nilikataliwa. Kampuni ya KFC ilipokuja China kwa mara ya kwanza, tulioomba kazi tulikuwa 24 na nilikuwa mtu pekee niliyetoswa. Nilitaka kujiunga na polisi na kutoswa mara 5, nilikuwa mtu pekee niliyekataliwa. Nilituma maombi mara 10 ya kurudi Chuo Kikuu cha Harvard, USA, lakini nilikataliwa.”

Kuna hali unaweza kupitia ukapata na hofu kuu na kujiuliza haya maisha ninaenda wapi? Kwa nini mimi Mungu? Kichwa kitakuwa na maswali mengi pasipo majibu.

Pengine utapata majibu ya sio sahihi. Kwenye harakati za maisha kuna kufeli kuna kukataliwa kila kazi ukiomba.

Kila mchongo ukifanya mchongo unakutosa mchana kweupe unabaki na maumivu yako. Unapopitia haya usiache kujiuliza unafeli wapi usiache kujifunza mbinu za mchezo.

Kumbuka maisha ni mchakato wa kujifunza. Pania kuwa bora , jifunze jifunze. Usibaki vilevile leo kama jana kama juzi ongeza thamani kwenye maisha yako ongeza thamani kwenye unachokijua ongeza thamani kwenye unachokifanya. Mwisho utafanikiwa.

Imeandaliwa na @tujuavyo na @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents