Michezo

Callum Wilson ameanza mazoezi baada ya majeraha ya muda mrefu – Howe

Meneja, Eddie Howe amesema kuwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Bournemouth, Callum Wilson amerejea tena katika mazoezi baada ya kusumbuliwa na majeraha ya goti kwa muda mrefu lakini hata hivyo atahitaji muda kuwa fiti zaidi.

Wilson mwenye umri wa miaka 25 alipata jeraha hilo katika mguu wakushoto mwezi Februari ikiwa ni sawa na majeraha aliyopata hapo awali katika mguu wake wa kulia mwaka mmoja uliyopita.

Akiwa ameonekana katika michezo ya Ligi Kuu nchini Uingereza mara 33 ikiwa ni zaidi ya misimu miwili, Wilson hajapewa muda maalumu wa yeye kuwa sawa lakini mwenyewe amesema kuwa yupo fiti.

“Hatakama ameanza mazoezi tutampa muda wa kutosha kadri atakavyo hitaji, anahitaji michezo mingi zaidi ilikuwa fiti ndipo tutampatia nafasi ya kucheza katika kikosi ,” Howe ameiyambia the Daily Echo.

Eddie Howe ameongeza “Anaonekana anaendelea vizuri na utimamu wa mwili unaendelea vizuri na hata kisaikolojia yukovizuri nafikiri amefikia katika hatua nzuri “.

“Kwa mchezaji ambaye amekuwa nje kwa kipindi kirefu nilazima atachukua muda kurudi katika kiwango na hilo ni jambo la kawaida.”

Bournemouth iponafasi ya 19 katika msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa kuwa na pointi 3 katika michezo sita iliyocheza huku ikiwazidi klabu ya Leicester City ambayo inaburuza mkia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents