Burudani

Cassim adai kuzipa exclusive TV za nje kabla ya nyumbani si kitu kizuri

Hitmaker wa Subira, Cassim Mganga amesema haoni kama ni ufahari kupeleka video yake ikaoneshwe kama exclusive kwenye vituo vya runinga vya nje na kuwaacha watanzania wengi wakisubiria.

Kassim Mganga

Akizungumza na Bongo5, Cassim amesema haoni uzito wa suala hilo kama ambavyo wengine wanavyolichukulia.

“Mimi na video yangu ya Subira nilisema nisianzie huko, kwanini mtu upate exclusive huko ndio uonekane kwamba wewe unakwenda kimataifa?” amehoji.

“Hata hapa nyumbani ni kimataifa vile vile wanaweza wakakuona. Kwa sababu kama watu wanatoka huko Nigeria na nchi nyingine wanatamani kuja bongo kufanya show au nyimbo zao zipigwe, kwanini sisi tusivujie nyumbani? Kwahiyo mimi nikasema huu wimbo lazima uanze nyumbani na process nyingine zitafuata tu,” ameongeza.

Kwa upande mwingine Cassim amewashukuru mashabiki wa muziki wake kwa kuonesha kuipokea kwa mikono miwili video ya wimbo wake Subira.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents