Michezo

Chama, Mkude na wengine wawili wajadiliwa kwa utovu wa nidhamu, Simba yasubiri majukumu yao ya taifa yapite

Mabingwa wa tetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC yatoa ufafanuzi juu ya tuhuma za utovu wa nidhamu za wachezaji wake wanne baada ya kushindwa kujiunga na timu hiyo kwenye mechi zake za Kanda ya Ziwa huku ikikana kuwasimamisha.

Wachezaji waliyotajwa na kikao hicho cha ndani ni Jonas Mkude, Gadiel Machael, Erasto Nyoni na Clatous Chama ambao kwa mujibu wa taarifa hiyo wanasubiriwa mpaka watakapo toka kwenye majuku ya timu za Taifa.

Tarehe 3 mwezi huu wa Oktoba siku ya Alhamisi klabu ya Simba ilifanya kikao chake cha ndani cha nidhamu na wachezaji hao waliyotajwa.

Nyota hao wamejikuta wakiingia kwenye sakata hilo kwa kushindwa kujiunga na timu katika mechi zake za Kagera Sugar dhidi ya Simba SC iliyopigwa Bukoba Septemba 26 na ule wa Biashara United uliyopigwa Musoma Septemba 29.

Kamati hiyo imekana taarifa za uongo zilizoenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa wachezaji hao wamesimamishwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kufanya shughuli zozote za klabu. Huku ikisema kuwa itawasubiri wachezaji hao kumaliza majukumu yao ya taifa ili kulimaliza sakata hilo.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents