Burudani

Cheche za Feza Kessy zaanza kuonekana katika jumba la Big Brother, apata bahati ya kuwa mkuu wa nyumba

Huwa wanasema nyota njema huonekana asubuhi, na asubuhi ya shindano la Big brother “The Chase” ilikuwa jana (May 27) ambapo nyota njema ya Feza ilionekana baada ya kupata cheo cha kuwa mkuu wa nyumba (Head Of House) katika Big Brother.

Feza_Lg_74d1aab9-1a24-4e1d-bbad-f477f8add475_021327180209007

Jana (May 27) ikiwa ndio siku ya kwanza kati ya siku 91 za shindano hilo, ilikuwa ni mwanzo mzuri sana kwa mmoja wa wawakilishi wa Tanzania Feza Kessy baada ya kupata cheo hicho cha kuiongoza Diamond House.

Moja ya ukubwa wa cheo hicho cha Feza kama kiongozi wa nyumba ni uwezo wa kumuokoa mshiriki aliyekuwa nominated kutoka na kumweka mshiriki mwingine katika eviction.

Shindano la big brother linahitaji Technics nyingi kwa kila mshiriki ili aweze kuonekana na kusikika zaidi ya wenzake , kitu ambacho kinasaidia kuchukua attention ya watazamaji wengi ambao mwisho wa siku wao ndio hupiga kura .

Uchaguzi wa mkuu wa nyumba ya Diamond ulifanyika kwa washiriki wote kuchukua mpira mmoja ulioko katika box lililowekwa garden bila kuangalia na yeyote atakayechukuwa ‘winning ball’ ndio mshindi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents