Burudani

Chidi Benz akiri kuwa muziki kubadilika, aahidi kurudi kwa kishindo

Rapper Chidi Benz amedai kuwa bado ana nafasi ya kufanya vizuri kimuziki licha ya muziki kubadilika na kuwa na ushindani mkubwa.

Chid-Beenz_full-2222

Chidi ameiambia Bongo5 kuwa amegundua anachotakiwa kufanya kwa sasa ni kufanya kazi kwa bidii tu.

“Naona nafasi yangu ipo sawa, bado nina nafasi kwenye muziki huu,” amesema. “Sema muziki sasa hivi umebadilika sana, watu wanafanya muziki mzuri na kwa ushindani, kwahiyo mimi pia nitafanya muziki mzuri wa ushindani. Nimejipanga vizuri, sasa hivi nimesharekodi na ninajiandaa kutoa ngoma mpya,” aliongeza.

Katika hatua nyingine Chidi Benz amedai kuwa video ya wimbo wake ‘Mpaka Kuche’ aliowashirikisha Diamond na AY itakuwepo.

“Kazi zangu mimi na Fid bado tunarekodi, kwahiyo tukimaliza kurekodi ndio tutajua inatoka lini. Pia tupo kwenye mikakati ya kufanya video ya wimbo ‘Mpaka Kuchee’ tutafanya na Adam Juma, kwahiyo watu wasubiri kazi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents