Habari

Chifu, polisi wanne wauawa na wezi wa mifugo Kenya

Takriban watu 11, wakiwemo polisi wanane na chifu, wameuawa katika eneo lenye ukame kaskazini mwa Kenya na wezi wa mifugo ambao walikuwa wakiwafukuza.

Wizi wa mifugo au ugomvi kuhusu malisho na vyanzo vya maji hutokea mara kwa mara kati ya jamii za wafugaji kaskazini mwa Kenya.

Jeshi la Polisi limesema kupitia ukurasa wa Twitter kwamba wizi huo wa mifugo umefanyika katika kaunti ya Turkana siku ya Jumamosi.

Polisi waliouawa walikuwa wakiwafuata watu wa kabila la Pokot ambao walivamia kijiji na kukimbia na ng’ombe.

Mnamo Novemba 2012, zaidi ya polisi 40 waliuawa katika shambulizi la kuvizia walipokuwa wakiwafuatilia wezi wa mifugo huko Baragoi, kaskazini mwa Kenya.

Mwaka 2019, takriban watu 12, wakiwemo watoto watatu, waliuawa katika mashambulizi mawili kaskazini mwa Kenya na wezi wa mifugo wanaoshukiwa kuwa wa kabila la Borana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents