Burudani

Christian Bella aeleza furaha yake baada ya muziki wake kuchezwa kwenye runinga kubwa za Kongo

Mwanamuziki Christian Bella amesema kuwa kitendo cha nyimbo zake kuchezwa kwenye runinga kubwa za Kongo kitawaziba midomo baadhi ya wasanii wa muziki wa dansi ambao walikuwa wanadai muziki wake anacopy kwa wasanii wa Kongo.
Christian Bella

Mkali huyo wa masauti ambaye nyimbo zake kwa sasa zinachezwa mara kwa mara kwenye runinga za Kongo, ameiambia Bongo5 kuwa nyimbo zake kuchezwa kwenye runinga kubwa za Kongo ni hatua nzuri katika muziki wake.

“Muziki wangu sasa hivi unazidi kupata nafasi nyumbani DRC Kinshasa nilipozaliwa mimi. Kwangu mimi ni furaha sana, kuna wasanii wenzangu wa muziki wa dansi ambao walikuwa wanadai mimi ninakopi muziki wa Kongo alafu nakuja kuimba huku,” alisema Christian Bella. “Lakini mimi najua kwamba ningekuwa nakopi muziki wawatu, sidhani kama ningepata airtime Kinshasa na wakapromote ngoma zangu kwa sababu napita kwenye vipindi vigumu sana, ni vipindi ambavyo vinawapromote mastaa wakubwa wa Kinshasa na hao watangazaji ni watangazaji ambao wanajua muziki ningekuwa nazingua wasingenipa support,”

Aliongeza, “Mimi naamini hakuna msanii mwenye muziki wake, kila kitu ambacho tunafanya leo tayari kuna watu huko nyuma walishafanya. Hakuna mtu anaweza kusema huu ni muziki wangu binafsi, muziki wazee wameshafanya kila kitu, sisi tunaboresha tu muziki, kipaji chako na akili yako ndio kitu kitaweza kuboresha muziki. Lakini huwezi sema hii style ya kwangu binafsi, hata wasanii ambao wapo Kongo pale, wanafanya vitu ambavyo watu walifanya kipindi cha nyuma. Mimi najua na mkitaka nitawaambia msanii fulani anaiba style ya Koffi, kwa sababu ni kawaida hata Kongo wanaonaga poa,”

Pia muimbaji huyo amedai hata wasanii wakongwe kama akina Koffi waliiga style za wasanii wazamani lakini wakaziboresha na kuwa za kuvutia zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents