Habari

‘Chungu’ iliyoshinda tuzo za ZIFF hatimaye kuingia sokoni


Filamu iliyoibuka kidedea kwenye tuzo za tamasha la kimataifa la filamu la Zanzibar, ZIFF, mwaka 2012 iitwayo ‘Chungu’, inatarajiwa kuingia sokoni Jumatatu hii. Filamu hiyo ilikuwa nje ya nchini ili kupikwa zaidi na kuipa ubora wa kimataifa na sasa ipo tayari kuingia sokoni.

Chungu itapatikana kwenye maduka ya jumla na reja reja.


Mtayarishaji wa filamu hiyo, Vicensia Shule ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sanaa na Sanaa za maonyesho, amesema filamu hiyo inayohusu maisha ya kawaida ya jamii ya Kitanzania na imerekodiwa katika vijiji mbalimbali vilivyopo Bumbuli mkoani Tanga.

Amesema anaamini itafungua milango kwa filamu bora na nzuri zisizo na wasanii nyota iliyobeba hadhi ya kimataifa.

“Tumefanya hivi ili kuwapa uhalisia wapenzi wa filamu zetu ambao ni wale wanaoishi katika makazi ya kawaida tu, hivyo naamini wataipenda sana na kujifunza mengi kupitia filamu hii”, alisema.

Chungu ni filamu ya pili ya Bi. Shule ambayo aliifanya kama sehemu ya utafiti katika masuala ya filamu nchini na amesema aliamua kuingia katika fani hiyo ya uaandaaji wa filamu ili kufahamu changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia ya filamu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents