Burudani

Cpwaa asaini na Universal Music Group, msikilize hapa akifafanua mkataba huo ulivyo (audio)

Rapper Ilunga Khalifa aka Cpwaa amesaini mkataba na lebal kubwa duniani ya Universal Music Group tawi la Afrika Kusini.

cpwaa3

Kupitia mkataba huo, kazi za Cpwaa zitakuwa zikisambazwa kupitia app maalum Kleek, iliyopo kwenye smart phone za Samsung katika nchini za Ghana, Angola, Kenya, South Africa and Nigeria.

Akielezea mkataba huo, Cpwaa ameiambia Bongo5, “Ni njia moja wapo ya kupata kipato kwasababu Afrika nzima mtu popote pale anakuwa na uwezo wa kusikiliza na kudownload nyimbo zako na pia vile vile ni marketing kubwa kwasababu UMG ni kampuni kubwa, ukifanya nao mkataba kama hivi wanakufanyia marketing hata ukiwa na nyimbo zako mpya wanakupa fursa mpya.”

Cpwaa amesema kwa kuanzia nyimbo zitakazokuwa zikisambazwa ni tano ambazo ni Problem, Jambo, Action, So Pwaa na 6 in the Morning. “Mkataba ni wa mwaka mmoja lakini kila mwaka unakuwa reviewed wanaangalia pia na mapato yako, uuzaji wako, trend yako nzima kuna vitu vingi vinahusika, amesema Cpwaa.

“Mimi mwenyewe nimekuwa very shocked, lakini naamini hiyo yote ni kutokana na juhudi zangu. Sio UMG tu, tayari nimeshakuwa approached na makampuni karibia mawili ya South Africa wanataka kunifanya distribution. Kwahiyo ni vile juhudi zangu na kazi zangu za siku ya nyuma na ambazo nazifanya mpaka sasa hivi naamini ndio zinanifungulia hii milango ya ridhiki. Na pia inajulikana vizuri sana hata watu wa Channel O wanafahamu katika moja ya wasanii ambao wako aggressive na wako very good in communication and persistent yaani ukikitaka kitu unakipata hapo hapo ni mimi hapa, nadhani hivyo ni vitu vilivyowaimpress.”

Msikilize zaidi hapa.

Hongera sana Cpwaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents