Michezo

Dani Alves: Kinacho wanyima mafanikio Arsenal ni wachezaji makinda na hivyo kukosa wazoefu

Beki Dani Alves wa Barcelona, Kuelekea mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora, amesema wapinzani wao Arsenal wanakosa uzoefu ndiyo maana wanashindwa kupata mafanikio na kushinda mataji kwa wingi.

Dani-Alves

Kikosi hicho cha Arsene Wenger kitakuwa mwenyeji wa Barcelona katika mechi ya kwanza ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Jumanne usiku, na kauli hiyo ya Alves. Alizungumza na gazeti la The Times, Alves alisema kikosi hicho cha Wenger kimejaa wachezaji chipukizi na hivyo kukosa wazoefu ambao ni muhimu ili kupata mafanikio.

“Katika Premier League wanaanza vizuri, lakini wanashindwa kubaki katika ‘levo’ hiyo na kutwaa mataji. Wanacheza mpira vizuri sana na wamejipanga vizuri kimbinu, lakini hakuna mchanganyiko wa vijana na wazoefu. Vijana wanataka kushambulia, lakini kuna wakati unatakiwa kuwa na uwezo wa kumiliki mchezo,” alisema Alves.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents