Burudani

David Beckham akanusha uvumi kuwa ana mpango wa kuigiza kama James Bond

Mwakilishi wa mchezaji mstaafu wa soka wa Uingereza, David Beckham ameiambia Daily Mail kuwa staa huyo hana mpango wowote wa kuigiza kama James Bond.

beckham

Winga huyo wa zamani wa Manchester United amekanusha ripoti zilizosambaa kuwa ana mpango wa kugombea nafasi ya kuigiza kama James Bond mwakani, licha ya kuwa mashabiki wamejaribu pia kumuomba afanye hivyo.

Pamoja na kutokuwa na mpango wa kuigiza kama James Bond, Beckham ambaye ni baba wa watoto wanne ataonekana kwenye filamu ya ‘Knights of the Roundtable: King Arthur’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents