Burudani

Shilingi milioni 12 zimetumika kutengeneza video mpya ya Belle 9

Belle 9 amesema video ya wimbo wake Shauri Zao aliyofanya na Hanscana imemgharimu shilingi milioni 12.

Belle9

Amesema hiyo ndio video yake ya kwanza kutumia fedha nyingi.

“Hii itakuwa tofauti kwa sababu video hii ina maandalizi makubwa, ina bajeti kubwa na pia imechukua muda mrefu kuishoot,” Belle ameiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Pia hii nimefanya na kampuni yangu ndio imesimamia kila kitu. Tofauti ya bajeti hii imekwenda kama milioni 12 hivi kwa sababu director peke yake tumemlipa milioni 4. Video Queen tumemlipa milioni moja na location pamoja na masuala ya make-up ni kama milioni 7 fulani. Kwahiyo ndio kazi yangu kubwa ambayo inakuja.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents