Michezo

Dennis atoa sababu hizi za kushangilia staili ya Ronaldo ‘Siii’ baada ya kuiadhibu Madrid ndani ya Santiago Bernabeu

Mshambuliaji hatari wa Club Brugge, Emmanuel Dennis amezungumzia sababu ya yeye kushangilia magoli yake kwa staili ya aliyekuwa nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo baada ya kuwaadhibu nyumbani kwao katika dimba la Santiago Bernabeu.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 21 raia wa Nigeria alifanikiwa kufunga mabao mawili peke yake na kuufanya mchezo huo kwenda sare ya 2-2 dhidi ya Real Madrid kwenye michuano ya Champions League siku ya Jumanne huku akiwakumbusha machungu ya kumkosa Ronaldo baada ya kushangilia kwa staili ya ‘Siii’ ambayo hutumiwa Mreno huyo.

Emmanuel Dennis wheels away in celebration after scoring for Club Brugge vs Real Madrid

Dennis amesema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akivutiwa na nyota huyo raia wa Ureno ambaye kwa upande wake anamuona kama shujaaa hata staili ya ushangiliaji.

Man of the moment Dennis preparing to perform the Cristiano Ronaldo 'Siii' celebration

Baada ya kupachika bao, Dennis akijiandaa kwaajili ya kushangilia kwa staili ‘Siii’ kama ya Cristiano Ronaldo

The Nigerian took full advantage of Real Madrid 's fragile defence, causing havoc all night

”Siku zote nimekuwa shabiki wa Cristiano na sikufurahi kuona anaondoka Madrid,” Dennis ameyasema hayo baada kumalizika kwa mchezo huo.

Dennis insisted his side's brave showing at the Bernabeu was not down to luck, but tactics

”Hivyo nilipanga kusherehekea kwa staili hiyo kama ningefunga bao ndani ya Bernabeu na ndivyo nilivyofanya. Kila mtu alifikiria kuwa tungefungwa kirahisi, tulijiandaa kwaajili yao tuliamini hilo na tulkuwa na matumaini.”

Cristiano Ronaldo invented the now-famous 'Siii' celebration which he started at Real Madrid

Dennis akiwa na mwezake mchezaji wa Afrika Kusini, Percy Tau walikuwa mwiba mkali kwenye lango la Madrid.

”Tulijaribu kwa kadri ya uwezo wetu, tulijifunza vya kutosha na kuja hapa kuhakikisha Ramos na Varane wanakimbia muda wote,” aliongeza Dennis.

”Wao ni mabeki na kazi yao kama mabeki huwa hawapendi kukimbia, timu nyngi huja hapa na kunza kujilinda lakini sisi tualiachana na kujilinda na badala yake tulifanya kazi kama kichaa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents