Burudani

Diamond alikuwa anauza duka Magomeni, sijalipwa hata shilingi mia ya wimbo wa ‘kamwambie’- Bob Junior

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na muandaaji wa muziki nchini Tanzania, Bob Junior amedai kuwa kwa mara ya kwanza kuonana na Diamond Platnumz ilikuwa ni mitaa ya Magomeni jijini Dar es salaam akiuza duka la nguo na yeye ndiye aliyeanza kumuomba amsaidie kurekodi kwenye studio zake za Sharobaro Records.

Bob Junior

Bob Junior amesema kwa mara ya kwanza alipokutana naye alikuwa ana-rap lakini akamwambua aachane na huo muziki na ndio akarekodi wimbo wa nenda kamwambie.

Wakati nakutana na Diamond ilikuwa mtaani tu maskani pale Magomeni alikuwa anauza duka la nguo, ikawa kila nikipita anasema Bob bwana  nifanyie kazi, siunajua mimi nina roho tofauti ..! alikuwa ana-rap rap kwa akili yangu nikamwambia aachane na muziki huo yaani muziki wa ku-rap rap hapana tujaribu kuimba. Ndio akaja kamwambie ikawa kama ina U-RnB nikamwambia badilika kidogo imba Bongo Fleva zaidi, Then Alhamdulillah tukatoa wimbo ukawa mkubwa lakini kumbuka kwa wimbo huo kuwa mkubwa sijawahi kuchukua shilingi mia. Album yake yote iliyotoka nimelipwa nyimbo nyingine lakini Kamwambie sijataka nilipwe kwa sababu aliniomba na nikapenda anavyoimba so baraka zangu na baraka zake Mungu akaona kilio chetu, Diamond akawa mkubwa na mimi mkubwa na sharobaro ikawa kubwa.“amesema Bob Junior kwenye mahojiano yake na Wasafi TV.

Bob Junior ni moja ya Maproducer waliomsaidia Diamond Platnumz kabla ya kuwa na jina kubwa miaka ya nyuma na alishwahi kutengeneza Hit songs kadhaa ikiwemo Kamwambie na Kwetu Mbagala.

Related Articles

54 Comments

  1. Bob wenenda direct sema tu mdogo wngu nasebu kaka yko ninashida hi na hi sio kuanza kutugea hadith eti nimerecord bure kwan alikukaba au ulirazimishwa au ndo unataka kiki wewe komba uyo simba akikupa kiki utakufa

  2. Bob mbn unalalmika si kuna wakati ule ulisema kuwa atapotea kimzik alivyojitoa kwako…na baadae ukamwambia asitumie ata ilo jna la sharobaro….kwenye maisha usimdharau wa chin yako kwan hujui atakuw nan baadae…so bob kama unashida zako,kamlilie yey uko sio mitandaon

  3. Kumbe hapo hakuna shida Kama hakulipwa kwa wimbo mmoja tu akalipwa kwa nyimbo zingine nnachokiona wimbo nenda kamwambie ulikua kama ni mtaji kwa wote wawili,kwanza diamond kanufaika kupata kazi nyingi,pili sharobaro,pia wakanufaika pia kwa kuitangaza studio yao,niliposoma kichwa cha habar nilidhan jamaa analalamika kumbe alikua anazungumzia namna diamond alivyotoka,na namna sharobaro record ilivyopata jina kutokana na wimbo huo!!!

  4. Bob junior acha lawama, kwani sisi wakati mnakubaliana kufanya kazi tulikuwepo?! Kama mlikubaliana kutokulipana sisi tutajuaje, afu kazi za zamani wasanii wengi na ma-producer walikuwa wanafanya kishkaji tu na sio kibiashara sana, mziki umekuwa biashara miaka hii ya karibuni,,,,,,kwanza ukiachana na hilo la kutokulipa hela ya iyo nyimbo ata ivyo Bob junior watu walikutambua kupitia diamond kupitia nyimbo ya kamwambia na mbagala so unatakiwa kushukuru tu ata kwa iko kidogo, ulikuwa huimbi ila ukahamasika kuimba kwa sababu ya mond….acha kulalama kwa ishu ambazo zimepita hazina faida.

  5. Alichosema Bob Junior ambaye ndie alimuibua Diamond Platnumz kupitia wimbo wa Kamwbie
    .
    “Wakati nakutana na Diamond ilikuwa mtaani tu maskani pale Magomeni alikuwa anauza duka la nguo, ikawa kila nikipita anasema Bob bwana nifanyie kazi, siunajua mimi nina roho tofauti ..! alikuwa ana-rap rap kwa akili yangu nikamwambia aachane na muziki huo yaani muziki wa ku-rap rap hapana tujaribu kuimba. Ndio akaja kamwambie ikawa kama ina U-RnB nikamwambia badilika kidogo imba Bongo Fleva zaidi, Then Alhamdulillah tukatoa wimbo ukawa mkubwa lakini kumbuka kwa wimbo huo kuwa mkubwa sijawahi kuchukua shilingi mia. Album yake yote iliyotoka nimelipwa nyimbo nyingine lakini Kamwambie sijataka nilipwe kwa sababu aliniomba na nikapenda anavyoimba so baraka zangu na baraka zake Mungu akaona kilio chetu, Diamond akawa mkubwa na mimi mkubwa na sharobaro ikawa kubwa.“amesema Bob Junior kwenye mahojiano yake na Wasafi TV.MAPOVU NA LINK JAMANI 😂😂 NAJUA TEAM WCB TUNAMFATAA HUKO

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents