Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariMahojiano

Diamond kwa sasa sio level za Wizkid, Burna boy na Davido ila alikuwa level moja

Kupitia kipindi cha RECAP & MANDO @el_manndo_tz ametoa maoni yake na kusema kuwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva Diamond platnumz kwa sasa kimuziki ameshuka, sio kama Diamond wa miaka mitano nyuma.

@el_mando_tz ameongeza kuwa Diamond ndio msanii pekee aliyekuwa kutoka Afrika Mashariki aliyekuwa anaiwakilisha kwenye Matamasha makubwa duniani, sio hilo tu Diamod ndio aliyeleta collabo kubwa na nyingi kutoka Marekani.

Kwa sasa Tamasha kubwa duniani la AFRO NATION linafanyika Miami nchini Marekani wasanii wengi ni kutoka nchini Nigeria ila Afrika Mashariki hakuna hata msanii mmoja.

Diamond ndio msanii pekee aliyekuwa annafanya show kwenye Tamasha hilo lakini kwa sasa hashiriki tena na hiyo yote inapelekewa na kutokufanya vizuri kwenye muziki wa nyumbani.

@el_mando_tz ameongeza kuwa kama Diamond ataamua kusimama kufanya muziki kwa sasa huenda tukauona muziki wetu ukashuka kama vile bongo movie ilivyoshuka baada ya Kanumba kupoteza maisha.

Uchambuzi mzima upo kwenye akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

Host: @@el_manndo_tz

Editor: @sameeer2_

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents