Habari

DRC: Yadaiwa takribani wafungwa 45 wamefariki kwa kukosa matibabu, Fahamu zaidi

DRC: Yadaiwa takribani wafungwa 45 wamefariki kwa kukosa matibabu, Fahamu zaidi

Wahudumu wa afya katika gereza moja mjini Bukavu mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasia ya congo wamesema kuwa wafungwa wapatao 45 wamefariki dunia tangu mwanzo wa mwaka huu kutokana na ukosefu wa matibabu. Wangonjwa wengine walipelekwa hosptali kuu lakini hakukua na huduma za kutosha.

Hali hiyo imewafanya timu ya madaktari katika gereza hilo kugoma kufanya kazi nakuomba serekali kuimarisha hali sio tu ya afya lakini pia ya maisha mazuri kwa wafungwa maeneo hayo.

”Tunachoomba kwanza ni hali ya wafungwa na haki yao iheshimiwe.wafungwa wanayo haki kiafya.” Alisema daktari mkuu wa kituo cha afya katika gereza kuu la Bukavu Bi Pamela Muhindo.

”Ikiwa serekali iliona ni vyema kuweka bodi la madakatari katika jela hiyo ili kuwatunza wafungwa vivyo hivyo wanapaswa kuweka vifaa muhimu kwa ajili yao.” aliongeza.

Gereza la Bukavu

Daktari huyo mkuu pia anasema wameamua kugoma kufanya kazi katika gereza hilo kutokana kutolipwa mishahara yao.

Lakini kikubwa ni hali mbaya ya huduma ya sio tuu ya afya bali pia mateso mengine wanayopitia wafungwa katika magereza wakiomba serikali kuboresha hali hiyo.

Tangu mwezi Januari mwaka huu hadi sasa zaidi ya wafungwa 45 wamefariki dunia kutokana na ukosefu wa matibabu katika gereza hilo.

Hata hivyo wafungwa 325 wanaugua ugojwa wa utapiamlo, 13 wakiwa na virusi vya HIV huku 23 wakiugua ugonjwa wa kifua kikuu.

Wanaharakati wa haki za kibinadamu wamesema kuwa lazima serekali isikilize wauguzi hao wa gereza hilo na kuchukua hatua za haraka.

Hali ya wafungwa sio mbayo katika jimbo la Bukavu pekee bali ni changamoto inayokabili sekta nzima ya afya nchini humo.

”Hali ya wafungwa hapa nchini sio yakuridhisha”,alisema mmoja wa wanaharakati hao.

Ramani ya BBC

Gereza kuu katika mji wa Bukavu lilijengwa kwa ajili ya wafungwa 500 pekee ,lakini kwa sasa gereza hilo linahifadhi zaidi ya wafungwa 1300.

”Huduma za afya,chakula pamoja na malazi ni changamoto kubwa inayowakabili wafungwa hao” alisema.

Kwa mujibu wa BBC. Ripoti mbalimbali zinasema kuwa idadi ya wafungwa wanaoteswa inazidi kupanda ikiwema mateso ya kikatili ikiwemo mateso ya kimwili na kimaadili huku askari polisi na askari jeshi ndio wanatajwa kutekeleza mateso hayo.

Hivi majuzi kanda moja ya video ilisambaa kwenye mitandao ya kijami ikionyesha zaidi ya wafungwa 17 wakiwa wamefariki kutokana na ukosefu wa chakula katika gereza la Kabare kusini mwa mji wa Bukavu.

Hali hiyo husababisha wafungwa kutafuta mbinu mbadala ili kujiokoa wakitumia njia za kutoroka jela.

Mpaka sasa hakuna afisa kutoka serekalini aliyezungumzia suala hilo Lakini BBC inaendelea kuwatafuta maafisa hao.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents