Burudani

Dully Sykes: Nina mpango wa kuujaza uwanja kama alivyofanya Cassper Nyovest Afrika Kusini

Ukizungumzia wasanii ambao wamekula chumvi nyingi au walikwepa mishale mingi ni pamoja na Mr Misifa, Prince Dully Sykes ambaye mpaka sasa anafanya vizuri.

Hit maker huyo wa ‘Inde’ ambaye anafanya vizuri kwa ngoma yake mpya ‘Yono’ aliyotumia neno la kiganda lenye maana ‘Ndio huyu’ kazungumzia ujio wa show yake ya uwanjani kama ile iliyofanya na Rapper Cassper Nyovest wa Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka jana.

“Wakitokea sponsors nataka kuifanya hiyo show ni show kubwa,” Dully amekiambia kipindi cha Zero Planet kupitia Ice FM.

Alipoulizwa sababu ambayo imempelekea kufikiria kufanya show uwanjani, staa huyo amesema, “wasanii wakubwa wote wanafanya hivyo, na mimi ni msanii mkubwa nchini kwangu nina sababu ya kufanya hivyo kujaza watu.”

Kwa upande wa collabo na wasanii international, Dully anasema tayari ameshafanya ngoma na Diamond Platnumz pamoja na Vanessa Mdee.

Na Gami Dee (Ice Fm)
Instagram: @gamideetz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents