Burudani

Eddy Kenzo aeleza sababu za kwanini BET walimkabidhi tuzo yake kwenye Red Carpert

Msanii wa Uganda aliyeshinda tuzo ya 2015 BET Viewer’s Choice Best International Artist, Eddy Kenzo ametoa maelezo ya kwanini alikabidhiwa tuzo yake kwenye Red Carpet.

Eddy kenzo

Licha ya kuwa wasanii wa Afrika na UK wamekuwa wakibaguliwa kwenye tuzo hizo kwa kupewa tuzo zao muda tofauti kabla ya tukio lenyewe, lakini mambo yalikuwa tofauti zaidi kwa msanii wa Uganda, Eddy Kenzo ambaye alikabidhiwa tuzo yake nje kabisa kwenye Red Carpet.

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo cha runinga hivi karibuni, Kenzo amesema kuwa waandaaji wa tuzo za BET walimfahamisha kuwa tuzo ya kila kipengele ilikuwa na mdhamini, na kampuni iliyodhamini tuzo ya kipengele chake haikulipia muda wa jukwaani na ndio sababu ya kukabidhiwa kwenye Red Carpet.

Ameongeza kuwa licha ya kutopewa tuzo ukumbini, lakini alithaminiwa vizuri katika mambo mengine kama wasanii wengine, ikiwa ni pamoja na kuwekwa hotel moja na mastaa kina Nicki Minaj, Drake na Tyga.

“Its upon the sponsors of the particular BET Award to pay for stage time. But otherwise I was treated well because I was sleeping in the same hotel with Drake, Tyga and Nicki Minaj,” alisema Eddy Kenzo.

Source: 411 UG

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents