Burudani

Familia ya Mbaraka Mwinshehe yadai haijanufaika na kazi alizoacha ndugu yao

Familia ya msanii mkongwe wa zamani kutoka mkoani Morogoro, Mbaraka Mwinshehe, imedai haikunufaika na kazi za mwisho ambazo aliacha ndugu yao.
Mbaraka+Mwinshehe

Muimbaji huyo wa zamani ambaye bado kazi zake zinaendelea kuishi, alifariki kwa ajali ya gari tarehe 12 Januari 1979 akiwa na umri wa miaka 34.

Akizungumza na BBC mke wa mwanamuziki huyo, Bi. Amney Shadad amesema kama familia haijanufaika na kazi za Mbaraka.

“Mauzo ya nyimbo ya Shida ni wakati yeye amekwenda kurecord kabla hazijatoka kwa bahati mbaya akapata ajali akafariki. Lakini wimbo ulivyotoka uliuza sana, mpaka ikapata Golden Disc na nyimbo nyingine ikapata Silver Disc lakini nimejitahidi kuzifuatilia sikufanikiwa, nimezungushwa mpaka leo na hapa kwetu (Morogoro) nilikuwa nafuatilia wakati huo wizarani wanisaidie lakini hakuna msaada wowote, kwa hiyo zile tuzo zote zimepotea,” alisema Bi. Amney Shadad .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents