Bongo Movie

Filamu ya action ya Jimmy Mponda, ‘Double J Final’ kutoka hivi karibuni

Muigizaji mkuu wa filamu ya action ya Kitanzania iitwayo Double J, Jimmy Mponda amewataka wapenzi wa filamu zake za action kukaa mkao wa kula kwakuwa sehemu ya mwisho wa muendelezo wa filamu hiyo itaingia sokoni hivi karibuni.

a2 posterdouble j

Akizungumza na Bongo5 kwa njia ya simu jana muongozaji na muigizaji huyo kinara wa filamu hiyo, Jimmy Mponda, aka Jimmy Master au J Plus alieleza kuwa ndani ya filamu hiyo, Angel ameigiza kama mtumiaji wa madawa za kulevya akitumia jina la Kwapu.

“Koku na Kwapuwa wamefanya poa sana kwenye ujio huo wa ‘Double J Final,” alisema.

Jimmy aliyewahi kutamba na mfululizo wa filamu za Misukosuko part one, two na three , alisema sehemu ya kwanza, ya pili na ya tatu ya Double J ilitoka mwaka jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents