Burudani

G-Nako aeleza ujumbe uliomo kwenye ‘Mavijana’ na ‘Chunga Sana Unyumba’

Rapper kutoka wa Weusi, G-Nako amezungumzia wazo la kutunga nyimbo zake mbili alizozitoa kwa pamoja ‘Chungu Sana Unyumba’ aliowashirikisha Barnaba na Lord Eyez na ‘Mavijana’ aliomshirikisha Nick wa Pili.

Gnako Insta

G Wara Wara amesema lengo la kuandika nyimbo hizo ni kufanya kazi kama kioo cha jamii kwa kuhimiza mienendo bora ya maisha.

“Unajua jamii yetu ukiangalia ina matatizo mengi yanayosababishwa na masuala ya mahusiano, kama kila mtu akaamua kuchunga unyumba mambo yataenda vizuri,” amesema. “Ukiangalia magonjwa, ugomvi na mambo mengi yanasabishwa na kutokuwa waaminifu kwenye mapenzi. Kwahiyo watu wachunge unyumba ili mambo yaende poa. Hata huu wimbo mwingine ‘Mavijana’ kama nilivyo mimi na wewe lazima mmoja am-motivate mwenzake ili kufanya vitu vizuri ndio maana mimi na mwenzangu Nick wa Pili tunajaribu kutumia muda wetu kuwapa njia na kuwatia moyo, kutoa elimu kwamba kama sisi ni taifa la kesho lazima tuwe responsible kwa kila kitu. Kila kitu kinatuangalia sisi, sasa tukianza kuingia kwenye vitu vingine vya anasa, madawa ya kulevya inakuwa sio sahihi kwa sababu taifa letu na kizazi chetu kinahitaji nguvu zetu,” amesema G-Nako.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents