Michezo

Gamondi Yanga ninayoitaka ndio hii

Kocha wa klabu ya Yanga Miguel Gamondi baada ya kuibamiza klabu ya CR Belouizdad ya Algeria kipigo cha goli 4-0 ametoka hadharani na kusema “Uwezo ambao tumeuonyesha dhidi ya CR Belouizdad niche kiwango ambacho falsafa zangu zinataka tucheze. Tulicheza mpira mkubwa sana, kilikuwa ni kiwango ambacho kama kusingesimama kwa Ligi tulitakiwa kufikia muda haspa mrefu.

“Nimewaambia wachezaji wangu tunatakiwa kushika hapa na kuendelea kucheza kwa kiwango hiki zaidi, tukifanikiwa hilo hakuna ambacho kitazuia mafanikio yetu kwenye malengo yetu. hatupaswi tena kucheza chini ya hapa”.

Kikosi cha Yanga jioni ya jana walikwishaanza safari kuelekea Misri kwa mafarao AL Ahly mchezo hue ukiwa ni wa kukamilisha hatua ya makundi na ndio mchezo utakaoamua nani akae juu ya kundi D.

Mchezo huu utachezwa siku ya Ijumaa tarehe 1/3/2024 majira ya saa 1:00 Usiku nchini Misri.

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents