Michezo

Pacome aitaka robo fainali kwa hamu

Mpaka sasa kwa michezo iliochezwa ya kombe la Klabu Bingwa Afrika kiungo wa Yanga Zouzoua Pacome, amesema akilini kwake kwa sasa haiwazi AL Ahly, bali anafikiria timu watakayokutana nayo kwenye hatua ya robo fainali.

“Kwangu muunganiko ule umejenga kitu kikubwa sana ambacho hakitasahaulika lakini zaidi na kuhakikisha timu inapata matokeo hata kama nisipofunga mimi”.

“Kwa ukweli siwazi sana mechi dhidi ya AL Ahly imeshakwisha maana tumeshatinga robo fainali, mawazo yangu ni nani tutakutana naye katika robo fainali kwani kwa sasa timu zote ni bora ndio maana zimefika hatua hiyo.”

“Naongeza kasi ya kufanya mazoezi magumu ili kuweka mwili sawa huku tukijipanga na mchezo huo usiojulikana kwani sitamani kikosi chetu kiishe kwenye hatua hii ya robo fainali,” Alisema Pacome ambaye amehusika katika mabao matano na akifunga matatu na kutoa asisti mbili.

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents