Michezo

Ngoma aipania Jwaneng Galaxy

Kiungo  mwenye asili ya DR Congo Fabrice Ngoma ambaye alisajiliwa dirisha kubwa ni mchezaji mwenye uzoefu zaidi katika michuano hii ya Klabu Bingwa Afrika kutokana na rekodi kali alizonazo na timu alizowahi kuchezea, amefunguka namna watakavyowanyanyasa Jwaneng Galaxy ya Botswana ikiwa ni mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Uzoefu wa Kiungo huyo ambaye amecheza mechi 13 kati ya 15 katika ligi kuu Tanzania Bara Ngoma amesema “Tunakwenda kucheza mechi ambayo wachezaji wote tunatakiwa tuiamue, sio sawa mpaka sasa timu kubwa kama Simba kushinda mchezo mmoja mpaka sasa lakini sisi ndio tumebeba matumaini ya Simba kama wachezaji.”

Ngoma aliendelea na kusema  “Ni sisi tuamue kufanya makubwa ili tuweze kutinga hatua inayofuata kwa ushindi mkubwa ambao utarejesha nguvu kwenye kikosi na Kocha kwa ujumla, kuwa makini na kutumia nafasi zote zitakazopatikana ndio zinazoweza kuamua mchezo maana tupo uwanja wa nyumbani mahala ambapo tunapafahamu vizuri hatutafanya makosa  tena.”

Mpaka sasa Simba na Jwaneng Galaxy zimekutana mara tatu katika ligi ya Mabingwa Afrika kila timu ikiibuka na ushindi mara moja na sare mara moja.

Wekundu wa Msimbazi kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Afrika wamefanikiwa kushinda mechi moja tu mpaka sasa hivi kati ya tano alizocheza kwa sasa Simba ana alama 6 huku kinara akiwa ASEC Mimosas na alama 11 mchezo wa jumamosi ndio utakaoamua hatima yao katika Michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Mchezo huu unatarajiwa kupigwa siku ya Jumamosi tarehe 2/3/2024 majira ya saa 1:00 Usiku.

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents