Burudani

Geo Poll: Clouds FM/TV zaendelea kuongoza kwa kusikilizwa/kutazamwa zaidi Tanzania

Kampuni maarufu kwa utafiti wa vyombo vya habari, Geo Poll, imetoa ripoti ya robo ya nne ya mwaka 2016 inayoonesha usikilizwaji na utazamwaji wa redio na TV.

Ikitumia taarifa ambayo huikusanya kila siku, Geo Poll imebaini kwa upande wa redio Clouds FM bado inaendelea kuongoza mbali kwa kusikilizwa sana nchini huku ikiwa na usikilizwaji wa juu zaidi kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi jioni.

Nayo Radio Free Africa imekamata nafasi ya pili kwa kusikilizwa zaidi hususan kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 2. “Kuna ushindani mkali baina ya vituo vya redio wakati wa mchana,” imesema ripoti hiyo.

Katika vituo 10 vya redio, Clouds FM imeendelea kuchukua sehemu kubwa ya wasikilizaji, ifikayo 23.6% ikifuatiwa TBC Taifa yenye 7.5% na Radio Free Africa yenye 7.3%.

Kwa upande wa runinga, licha ya Clouds TV kwa ujumla kuwa kituo kinachotazamwa zaidi nchini, saa 2 usiku hadi saa 3 usiku (muda wa taarifa ya habari) ITV ndiyo inayotazamwa zaidi.

Clouds inachukua 19.6% ya utazamwaji ikifuatiwa na East Africa TV ikiwa na wastani wa 17.2% na kufuatiwa na ITV yenye 17.0%, huku TBC1 ikishika nafasi ya 4 kwa wastani wa 10.8%.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents