Burudani

Ifike kipindi serikali isikie kilio hiki cha wasanii na waongozaji video

Moja ya sababu zinazotolewa na wasanii kwenda kushuti video Afrika Kusini ni ugumu wa upatikanaji wa vitu hapa nyumbani.

Kupitia kipindi cha Ziro Planet ya Ice Fm, Msafiri Shabani ambaye ni director wa kampuni ya Kwetu Studios, ameungana na sababu zilizowahi kutolewa na Chege, Diamond na Madee kwenda kushuti video SA.

“Unakuta ni ngumu sana kufanya shooting kwenye nyumba ya serikali tu, mpaka upate kibali unakuta tayari nyumba ishapitwa na wakati wake,” amesema.

“Kwa mfano unataka kwenda kushoot kwenye mbuga au hifadhi japo tutakuwa tunatangaza hifadhi zetu unakuta charging zipo juu sana, endepo serikali ikitusapoti kua wasanii na mnaoshuti video fanyeni hivi ili tuweze kutangaza utalii wetu nafiri itakuwa kitu kizuri sana na hii wamefanya sana watu wa Brazil, Marekani sasa hizi wanataka sera ya Mmarekani kwanza na endapo tukifanya hivi tutatangaza utalii wetu,” aliongeza.

Na Gami Dee
Instagram: @gamideetz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents