Burudani

Gigy Money aiponza Wasafi Tv, yafungiwa miezi 6 (+ Video)

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekitaka Kituo cha Runinga cha Wasafi (Wasafi TV) kusitisha kurusha matangazo kwa miezi sita (6) kuanzia leo Januari 5, 2021.


Maamuzi hayo yanakuja kufuatia maudhui ya picha jongefu yaliyomwonesha msanii wa bongo Fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money akicheza ‘utupu’ kinyume na Kanuni katika tamasha la “Tumewasha Live Concert” lililorushwa Januari Mosi 2021 kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku.

Aidha Wasafi Tv wanatakiwa kutumia siku ya leo kuomba radhi kwa watazamaji wake kufuatia ukiukaji huo na wakikaidi hatua zaidi za kisheria na udhibiti zitachukuliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents