Burudani

GK adai Dogo Janja ndiye msanii wake bora kwa sasa ‘lazima nifanye naye ngoma’

Msanii mkongwe aliyewai kufanya vizuri na Kundi la East Coast Team, King Crazy GK amefunguka kwa kusema kuwa rapa Dogo Janja ndiye msanii wake bora kwa sasa.
dogo-janja

GK amesema anafurahishwa na jinsi rapa huyo anavyoweza kurap akiwa amerelax tofauti na wasanii wengine.

“Dogo Janja noma sana yule mtoto, nyimbo yake mpya inaitwa ‘Kidebe’, Dogo Janja ni rapa, angalia kwenye Kidebe alichokipanya, anarap yupo flexible. Yaani ana classics music,” GK alikimbia kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM.

Aliongeza, “Muziki ni kama ukishajua kuogolea unaweza ukapiga mbizi, unaweza kufanya chochote unachotaka, mimi amenivutia sana nitafanya naye kazi moja,”

GK kwa sasa anafanya vizuri na video yake mpya ya wimbo ‘Nzuri Pesa’ ambayo achia wiki mbili zilizopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents