Burudani

Hatuna nyota ya kutoa stori pembeni ndio muziki huende – ZaiiD

Rapper wa SSK, ZaiiD amewataka mashabiki kusikiliza muziki na siyo kusikilizishwa.

Akizungumza na Bongo5 na ZaiiD amesema kuna stori za nje ya muziki ambazo huwa zinalazimisha mashabiki kusikiliza muziki wa wasanii fulani hivyo wale wasio na utaratibu huo muziki wao haupati nafasi.

“Mashabiki wasikilize sana muziki na wasisikilizishwe, watu wengine hatuna nyota ya kutoa stori pembeni ndio muziki huende” amesema ZaiiD.

“Sisi wengine tunatoa muziki tu kwa hiyo kuwa wasanii wengi wana vipaji vya hali ya juu kwa hiyo wasapoti vipaji kadiri wawezavyo, hizo stori kama wanataka wazifuate kwa watu wenye stori,” ameongeza.

ZaiiD kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Wowowo’ pamoja na ile ya kundi lao la SSK, Slow Down.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents