Habari

Hatutaki vita baridi na China – NATO

Mkuu wa muungano wa Nato amewataka wanachama wa muungano huo kuzungumzia kuhusu kuimarika kwa China katika mkutano ulioitishwa ili kuonesha jinsi Marekani inavyounga mkono muungano huo wa mataifa ya Magharibi.

Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg anasema muungano huo hautaki vita baridi na China

Mkutano huo unatarajiwa kutoa taarifa inayoelezea tabia za China kama Changamoto kuu baada ya mkutano huo nchini Ubelgiji.

Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg alisema kwamba mkutano huo ulikuwa muhimu kwa muungano huo.

Ni mkutano wa kwanza wa Rais wa Marekani Joe Biden tangu alipochukua madaraka.

Nato ni muungano wenye uwezo mkubwa kisiasa na kijeshi kati ya mataifa 30 ya magharibi pamoja na yale ya Marekani kaskazini.

Ulibuniwa baada ya vita ya pili ya dunia ili kujibu kupanuka kwa uongozi wa kikomyunisti.

Katika miaka ya hivi karibuni , Muungano huo ulikumbwa na changamoto wakati viongozi walipojadili kuhusu lengo lake na ufadhili.

Hali ya wasiwasi iliongezeka wakati wa utawala wa rais Trump ambaye alilalamika kuhusu ufadhili wa taifa lake na kuhoji jukumu la Marekani kutetea washirika wake wa Ulaya.Rais wa Uturuki Reccep Teyyip Erdogan na mwenzake wa Marekani Joe Biden

Rais wa Uturuki Reccep Teyyip Erdogan na mwenzake wa Marekani Joe Biden

Badala yake , mrithi wake Bwana Biden ametaka kuimarisha uungwaji mkono wa Marekani kwa muungano huo wenye takriban miaka 72.

”Nataka kuweka wazi : Nato ni muhimu sana kwa maslahi ya Marekani” , bwana Biden alisema alipowasili katika mkutano huo siku ya Jumatatu.

Taifa lake lilisema kwamba, lilikuwa na jukumu la siri kuafikia kifungu cha 5 cha makubaliano ya Nato , ambayo yanashurutisha mataifa wanachama kujilinda dhidi ya mashambulizi.

Kwanini Nato inaiangazia China?

Kulingana na rasimu ya taarifa hiyo ilioonekana na vyombo vya habari , matarajio ya Uchina yaliyotajwa na tabia yake ya uthubutu inaleta changamoto za kimfumo kwa sheria ya kimataifa na kwa maeneo yanayohusiana na usalama wa muungano huo”Manuwari ya China

Rasimu hiyo inasema kwamba China inaimarisha kwa kasi uwezo wake wa kinyuklia mbali na uwezo wake wa kijeshi na piaa inashirikiana kijeshi na Urusi.

“Tuna wasiwasi na China kutoweka wazi mambo yake mbali na utumizi wa taarifa za kupotosha”, iliongezea.

Mshauri wa kitaifa wa rais Joe Biden , Jake Sullivan alisema kwamba mazungumzo ya Nato yataangazia usalama kwa ujumla ikiwemo kutoa upinzani mkubwa kwa China na kuimarika kwa jeshi lake.

”Hatuingii katika vita baridi na China sio mshirika wetu, na sio adui wetu”, bwana Stoltenberg aliambia wanahabari katika makao makuu ya Nato.

”Lakini tunahitaji kuangazia kwa pamoja kama muungano , changamoto zinazotolewa na kuimarika kwa China kwa usalama wetu”.

China ni mojawapo ya mataifa yenye uwezo mkubwa wa kijeshi na kiuchumi , ambacho chama chake tawala cha kikomyunisti kimeshikilia siasa maisha ya kila siku na jamii kubwa.

Nato imeendelea kuwa na wasiwasi kuhusu kuendelea kuimarika kwa China kijeshi hatua ambyo ni tishio kwa usalama na thamani ya demokrasia ya wanachama wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents