Michezo

Hawa ni makocha waliopata mafanikio makubwa duniani kwa muda wote

Timu ikiharibu uwanjani mtu anayetuhumiwa ni kocha, ndiyo maana wanasema ‘Coach are hired to be fired’.

5-8-13-Sir-Alex-Ferguson_full_600

Timu inapomsajili kocha wanakuwa wanatengeneza fikra kubwa juu ya kocha wao, wengine wanapeleka fikra zao mbali zaidi kwa kujijengea kuwa baada ya kumchukua huyo kocha makombe yote ya mashindano yaliyo mbele yao lazima wayachukue.

Kuna makocha wachache ambao dunia inawatambua kwa mafanikio yao waliyoyapata kwenye mpira, lakini hakuna mazuri yasiyo kuwa na vikwazo.

5. Walter Smith
walter-smith1

Kocha huyu ni raia wa Scotland, aliwahi kuzifundisha timu za Everton, timu ta taifa ya Scotland, Rangers, pia alishawahi kuwa kocha msaidizi wa Manchester United.

Walter Smith ni kocha ambaye hataweza kusahaulika kwenye historia ya timu ya Rangers na nchi ya Scotland kwa mafanikio ambayo aliyoweza kuyapata kipindi alipokuwa kocha. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 68 kwa sasa ameweza kuchukua jumla ya vikombe 21 alipokuwa na timu yake ya Rangers kama kocha mkuu.

Scottish Premier League: 1991, 1992, 1993, 1994, 1995, 1996, 1997, 2009, 2010, 2011 (10)
Scottish Cup: 1992, 1993, 1996, 2008, 2009 (5)
Scottish League Cup: 1993, 1994, 1997, 2008, 2010, 2011 (6).

4. Mircea Lucescu
831882_w2

Mirce Lucescu aliyezaliwa 29 July 1945, ni miongoni mwa makocha raia wa Romania ambao dunia haitaweza kuwasahau kutokana na mafanikio makubwa waliyowahi kuyapata kwenye mpira. Kocha huyu ambaye alizifundisha timu 12 tofauti za ligi mbalimbali duniani, Corvinul Hunedoara, Romania, Dinamo București, Pisa, Brescia, Reggiana, Rapid București, Internazionale, Rapid București, Galatasaray, Beşiktaş, Shakhtar Donetsk.

Lucescu amefanikiwa kupata jumla ya vikombe 21 kwenye maisha yake yote ya ukocha.

Dinamo Bucureşti
Liga I: 1990
Cupa României: 1986, 1990 (2)

Rapid Bucureşti
Liga I: 1999
Cupa României: 1998

Galatasaray
Süper Lig: 2002

Beşiktaş
Süper Lig: 2003

Shakhtar Donetsk

Ukrainian Premier League: 2005, 2006, 2008, 2010, 2011, 2012, 2013, 2014 (8)
Ukrainian Cup: 2004, 2008, 2011, 2012, 2013 (5)
UEFA Cup: 2009

3. Valeriy Lobanovskyi
Valeriy Lobanovsky

Ni miongoni mwa makocha wenye uwezo mkubwa kwenye ufundishaji na waliojipatia heshima kubwa kwenye ramani ya mpira wa miguu hapa duniani. Lobanovskyi alifariki 13 May 2002, akiwa na umri wa miaka 63.

Mafanikio makubwa aliyapata kocha huyu alipokuwa anaifundisha timu ya Dynamo Kyiv, japo aliwahi kuifundisha timu ya taifa ya Ukreni lakini dunia ilimtambua zaidi alipokuwa na Kyiv na kujikusanyia jumla ya vikombe 24 kwenye maisha yake yote ya ukocha.

Dynamo Kyiv
Soviet Top League: 1974, 1975, 1977, 1980, 1981, 1985, 1986, 1990 (8)
Ukrainian Premier League: 1997, 1998, 1999, 2000, 2001 (5)
Soviet Cup: 1974, 1978, 1982, 1985, 1987, 1990 (6)
Ukrainian Cup: 1998, 1999, 2000 (3)
UEFA Cup Winners’ Cup: 1975, 1986 (2)

2. Jock Stein
jock-steins-quotes-4

Jock Stein alikuwa raia wa Scotland, aliwahi kuzifundisha timu kama vile, Dunfermline Athletic, Hibernian, Scotland, Celtic, Leeds United, Scotland. Mwaka 10 September 1985 ndiyo kocha huyu alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 62.

Timu ya Celtic na dunia nzima haitaweza kumsahau kocha huyu ambaye alipata mafanikio zaidi alipokuwa na timu hiyo na kufanikiwa kuchukua jumla ya vikombe 25.

Hivi ni vikombe ambavyo kocha huyo amewahi kuvichukua akiwa na timu yake ya Celtic, timu hiyo imempatia umaarufu mkubwa sasa ni miaka 21 tangu amefariki lakini watu bado wanamkumbuka kwa yale makubwa aliyowahi kuyafanya kwenye mpira.

Celtic
Scottish First Division: 1966, 1967, 1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1973, 1974, 1977 (10)
Scottish Cup: 1965, 1967, 1969, 1971, 1972, 1974, 1975, 1977 (8)
Scottish League Cup: 1966, 1967, 1968, 1969, 1970, 1975 (6)
European Cup: 1967

1. Sir Alex Ferguson

2445298-3x2-940x627

Kocha huyu mwenye miaka 74 raia wa Scotland, ulimwengu mzima unamtambua mpaka Malkia wa Uingereza ndiyo maana aliwahi kumpa jina la ‘Sir’.

Anatambulika zaidi kama Sir Alexander Chapman “Alex” Ferguson, amepata mafanikio zaidi akiwa na timu ya Manchester United ambayo tangu ameanza kuifundisha amefanikiwa kuchukua vikombe vyote vya Uingereza na makombe ya Ulaya pia.

Timu alizowahi kufundisha kocha huyu ni, East Stirlingshire, St Mirren, Aberdeen, Scotland, Manchester United.

Kutokana na heshima yake yeye ndiyo kocha ambaye amechukua makombe mengi duniani, mpaka anastaafu ukocha mwaka 2013 alikuwa tayari ameshachukua makombe 35 kwenye maisha yake yote ya ukocha.

Aberdeen
Scottish Premier Division: 1980, 1984, 1985 (3)
Scottish Cup: 1982, 1983, 1984, 1986 (4)
Scottish League Cup: 1986
UEFA Cup Winners’ Cup: 1983

Manchester United
Premier League: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999, 2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013 (13)
FA Cup: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004 (5)
Football League Cup: 1992, 2006, 2009, 2010 (4)
UEFA Cup Winners’ Cup: 1991
UEFA Champions League: 1999, 2008 (2)
FIFA Club World Cup: 2008

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents