Habari

Helikopta kupelekwa mlima Kilimanjaro kusaidia kuuzima moto, Waziri Kigwangalla athibitisha moto kuwa mkubwa (+Video)

Serikali ya Tanzania inatazamiwa kutuma helikopta na ndege katika mlima Kilimanjaro nchini Tanzania kujaribu kuuzima moto unaoendelea kuwaka kwa siku ya saba sasa.

hayo ameyasema Waziri wa Maliasili na utalii Dkt Hamis Kigwangala baada ya moto kuendelea kuwaka katika mlima huo .

Jana Waziri Kigwangala alitangaza kuwa wameweza kuudhibiti moto huo, lakini baadaye moto huo ulisaambazwa zaidi na upepo uliovuma katika mlima huo.

Katika ujumbe wake wa Twitter Waziri Kigwangala amethibitisha kuwa moto unaendela kuwaka Katika mlima huo mrefu zaidi barani Afrika.

kwa kusema kuwa “kazini Mlimani Kilimanjaro jana. Bado tunahangaika na kuzima moto. Kazi ni ngumu na kubwa kuliko inavyodhaniwa. Changamoto ni upepo mkali na kukauka kwa nyasi na vichaka. Taratibu zikikamilika leo tutaweza kuanza kutumia Helicopters na ndege kuzima moto.”

 

https://www.instagram.com/p/CGXDATTBB1p/

sn

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents