Afya

Huduma ya puto la kupunguza uzito yafika Mwanza na Arusha (Video)

Waratibu  wa masuala ya upasuaji wa urembo au marekebisho mbalimbali katika mwili kutoka Plastic surgery Coordinators Tanzania  ambapo moja ya shughuli zao ni upasuaji wa urembo kama vile kuongeza au kupunguza maziwa au sehemu mbalimbali za mwili kwa wanawake, pia kupunguza maziwa kwa wanaume, kwa njia mbalimbali za kisasa yaani (breast Reduction/lift/augmentation)kunyanyua uso na shingo ama sehemu mbalimbali za uso (face and neck lift) kupandikiza nywele(hair transplant)  Huduma za kurekebisha masikio yaani (Otoplast)au marekebisho mbalimbali ya mwili yanayotokana na sababu mbalimbali kama vile marekebisho ya makovu mbalimbali ya moto, ajali, upasuaji holela(scar revision)

Pia huduma za kuondoa nyama sehemu mbalimbali za mwili kama tumboni (Tummy Tuck)au maeneo mengine ,pamoja na kuondoa mafuta mwilini kwakutumia vifaa na mbinu maalum za kisasa (Vaser Liposuction)pia huduma zakuhamisha mafuta yako kutoka sehemu moja ya mwili kwenda nyingine (fat Transfer/Fat Grafting) pamoja na huduma nyingine nyingi.

Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha madaktari na hospitali zinakidhi viwango vya kimataifa ikiwemo kupata taarifa sahihi za madaktari  tunaowatumia pamoja na takwimu sahihi za hospitali ikiwemo kiwango cha maambukizi  na idadi kamili ya vifo(infection and death rate). Pia tunasimamia malipo pamoja huduma za wateja wetu katika nchi atakayokuwa anapatiwa huduma .

Lengo letu la Kuwaita hapa leo ni kupenda kuwajulisha kuwa huduma  ya puto yaani (INTRAGASTRIC BALOON PROCEDURE) kwa sasa itakuwa inafanyika katika hospitali za  mikoani ikiwemo Seliani hospital Arusha, CF hospital Mwanza, Saifee Hospital Dar es salaam na  tutaendelea kuwapa taarifa za mikoa mingine.

Tumeendelea kuhakikisha huduma hii inapatikana sehemu nyingi zaidi ndani ya Tanzania ili kuruhusu ushindani wa bei ambao utawapa wateja wetu unafuu wa gharama na vilevile ili kuweza kuwafikia wateja wetu kwa urahisi zaidi.

Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Wizara yetu ya afya, lakini kipekee kwa Madaktari wetu wa hapa nchini kwani kwa kushirikiana nao kwa mara ya kwanza kabisa Tanzania mnamo tarehe 15 mwezi wa 11 mwaka jana tuliweza kuweka historia kwa kuratibu na  kupatia vifaa pamoja na kuratibu madaktari wetu kupata ujuzi wa ziada juu ya PUTO  na hivyo kufanikisha   hospitali yetu ya Taifa Muhimbili Mloganzila, kuweza kutoa huduma ya Puto .

 Lengo letu la kuhakikisha kuwa huduma hii inapatikana hapa nchini kwanza ni kutoa shukrani kwa watanzania ambao wao walituamini na kuchagua kutumia huduma zetu toka zilipoanzishwa. Vilevile kutokana na muitikio huo tulishauriana kuhakikisha kuwa huduma zote zinazofanyika nje ya nchi na zinazoonekana kuwa zinapatikana kwa gharama kubwa ,  tuhakikishe tunazileta nyumbani kwasababu tunaamini madaktari wetu na  kuwa tutashirikiana nao pamoja na wizara husika ili kuhakikisha  huduma  tofauti tofauti zinazohusiana na masuala ya afya na urembo  zinafanyika hapa nchini  ili kupunguza machungu ya gharama za nyongeza kama usafiri, malazi, chakula, muda na kutokuwa karibu na wapendwa wetu wakati wakupokea huduma hizo katika nchi nyingine.

Wito wetu ni kuwaomba watanzania kuamini huduma hizi mpya na kuendelea kuzifanyia hapa nyumbani , vilevile  kuwasihi watanzania kutumia huduma zetu ili kuepuka madhara makubwa ikiwemo kutumia hospitali na madaktari wa nje wasiokuwa na sifa wala mkataba wowote halali na mteja ambapo imepelekea watanzania wengi kuishia kupata madhara makubwa ya kiafya na hivyo kuleta usumbufu na vilevile gharama kubwa zaidi kwao.

Tungependa kuwashauri watanzania kuwa na utaratibu wakutumia kampuni mbalimbali zilizopo hapa nchini ambazo zinahusika na masuala ya uratibu wa wagonjwa na wateja wanaohitaji upasuaji wa masuala ya urembo (Medical , plastic and reconstructive surgeries coordinators),

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents