Habari

Idadi ya vifo vilivyotokana na mlipuko wa tenki la mafuta vyafikia 131, Sierra Leon

Vifo vilivyotokana na mlipuko wa tenki la mafuta Sierra Leone vimeongezeka na kufika 131 na wengine 63 wanatibiwa hospitalini.

Siku ya Jumatatu, idadi ya waliopoteza maisha ilikuwa ni 115 na 91 walikuwa wakipatiwa matibabu. Ajali hiyo mbaya ilitokea baada ya lori kugongana na tenki la mafuta Ijumaa iliyopita, katika eneo la viwanda mjini Freetown.

Wakazi wa eneo hilo walikimbilia kwenda kuchota mafuta yaliyokuwa yakichuruzika wakati tenki hilo lilipolipuka na kuwaunguza waliokuwa karibu nalo.

Rais Julius Maada alitangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Jumapili. Taifa hilo limeomba kuchangiwa msaada wa damu, madendeji, na dawa za kuwahudumiwa waliojeruhiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents