Habari

Intaneti yaendelea kukosekana Sudan

Huduma ya intaneti haijarejea nchini Sudan licha ya mahakama kuziamuru kampuni tatu kubwa za mawasiliano kurejesha huduma hiyo.

Sudan ilifunga huduma ya intaneti Oktoba 25 kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

Pia iliuondoa madarakani utawala wa kiraia uliyokuwa unaongoza taifa hilo katika kipindi cha mpito tangu kupinduliwa kwa Omar al-Bashir.

Mahakama moja Jumanne iliamuru kampuni za Zain, MTN na Sudani, kurudisha huduma za intaneti lakini shirika linalofuatilia uhuru wa matumizi ya intaneti la Netblocks, limesema kwamba bado hakuna huduma ya intaneti nchini humo.

Wanaharakati wa kudai mabadiliko, waliofanikiwa kuandaa maandamano ya awali, wamefanikiwa kuandaa maandamano ya kutaka kurejeshwa utawala wa kiraia bila ya kuwepo huduma ya internet. Wameitisha maandamano mengine Jumamosi, Novemba 13.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents