Michezo

Inonga alamba shavu

Klabu ya Simba kuelekea kwenye mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi klabu Bingwa Afrika wakiwa wanatafuta alama tatu kwa ajili ya kujihakikishia wanafuzu kuelekea hatua ya robo fainali leo katika mkutano na waandishi wa habari Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba Ahmed Ally amesema “Mgeni rasmi katika mchezo wetu dhidi ya Jwaneng Galaxy ni Henock Inonga Baka na tumeamua kumpa heshima hii kwa sababu ndiye mchezaji pekee katika ukanda wa mashariki na kati ambale amefikisha timu yeke nafasi ya nne kwenye michuano ya AFCON”.

Mchezo huu dhidi ya Jwaneng Galaxy Wekundu wa Msimbazi wanatakiwa kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu kuelekea robo fainali mpaka sasa bado hawana uhakikac wa kufuzu ikumbukwe mara ya mwisho Jwaneng Galaxy aliweza kumfunga Simba katika uwanja wake wa Benjamini Mkapa 3-1.

Ahmed Ally aliendelea na kusema “Anastahili kuwa mgeni rasmi, amefanya mengi na Taifa lake la Congo ameipa heshima kubwa Simba kupitia AFCON na sisi kama Simba cha kumlipa ni kumpa heshima kuwa mgeni rasmi”.

“Mechi kama hii ambayo tunakwenda kuicheza Jumamosi, Simba tumeshacheza mechi za aina hiyo tano (5) na zote tulipata ushindi, Hatujawahi kushindwa kupata ushindi katika mechi ya hatua kama hii ya kutupeleka hatua ya robo fainali, na Machi 2, 2024 tutaenda kuandika historia nyingine, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally”.

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents