Michezo

MO Dewji awapa msaada Yanga kwenda robo Fainali

Afisa Habari wa klabu ya simba Ahmed Ally, amegusia juu ya watani wao Yanga SC kutinga hatua ya Robo Fainali klabu bingwa Afrika kwa kusema kuwa safari ya Yanga SC katika soka la kimataifa Rais wa Heshima wa Simba MO Dewji alilipa msaada.

“Yanga kufuzu robo fainali wakupongezwa na kushukuriwa ni Rais wa heshima wa Simba Mohammed Dewji na wa pili kupongezwa ni Simba”.

“Simba na Mohammed Dewji tusingekuwa na maono ya kufika mbele kwenye soka la Afrika hakuna klabu ambayo ingefanya wanavyofanyawao leo sababu Mohammed Dewji ndiye aliyefanya timu nyingine ziamke”.

Mohammed Dewji wakati anaanza sera yake ya kuwekeza Simba SC alisema anataka Wekundu wa Msimbazi ichukue Ubingwa wa Afrika lakini wakati huo vilabu vingine vilikuwa vimelala usingizi wa Pono na walikuwa wameridhika kushindana humu kwenye Soka la Nyumbani” Ahmed Ally, Afisa Habari na mawasiliano wa Klabu ya Simba SC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents