Burudani

Jambo Squad wafungua mgahawa Arusha

Wasanii wa kundi la Jambo Squad kutoka Arusha wamethibitisha kauli ya kuwa muziki unalipa baada ya kufungua mgahawa jijini humo.

JamboSquad&Linex500

Jambo Squad wamedai kuwa licha ya kuonekana wanafanya muziki wa tofauti, wameweza kupiga hatua kimaisha.

“Sisi ni watoto wa uswahilini, tumelelewa uswahilini so maisha tunayajua,” waliiambia XXL ya Clouds FM.

“Sisi ni watu wa biashara sio kukaakaa tu. Ila kwa sasa hivi tumeamua tuanzishe sehemu ambayo itatukutanisha na watu wetu ambayo ni CafĂ©. Ni biashara ambayo itaingiza pesa kila siku, ndio tukaamua kufungua Cafe. Ipo maeneo ya Sakina, ambapo ni karibu na Jambo Squad Camp.”

Wamedai kuwa mgahawahi huo umewagharimu fedha nyingi kuuanzisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents