Burudani

Jay-Z na Solange Knowles waonekana pamoja wakifanya shopping ya pete baada ya video ya ugomvi wa kwenye lift kusambaa

Miongoni mwa habari zilizozungumziwa sana jana ni pamoja na ya video iliyovuja ikimuonesha dada yake Beyonce, Solange akimshambulia shemeji yake Jay Z kwenye lift. Baada ya video hiyo kusambaa, Jay Z na Solange walionekana wakifanya shopping ya pete katika duka moja huko New York, Jumanne (May 13).

Jay n solange

Kwa mujibu wa vyanzo, Jay Z na Solange walionekana wakichagua pete za kike katika duka hilo kwa dakika zipatazo 20, na inasemekana kuwa wote hawakuonesha kuwa na hasira japo walikuwa wakichagua kimya kimya.

Hata hivyo vyanzo hivyo vimesema waliondoka bila kununua chochote.

Jumatatu iliyopita TMZ iliweka video ikimuonesha mdogo wake Beyonce, Solange akimshambulia Jay Z kwa ngumi na mateke mara tu baada ya kuingia kwenye lift, habari ambayo ilipokelewa kwa hisia tofauti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents