HabariMichezo

Je, Nabi ajengewe sanamu akishinda mati yote matatu ?

Kikosi cha @yangasc kimewasili alfajiri ya leo kutoka Afrika Kusini ambapo waliwakabili Marumo Gallants kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Professor @nabinasreddine akiwa Afrika kusini amefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1 na hivyo kutinga fainali kwa (Agg 4-1).

Mbali na Fainali ya Shirikisho Afrika, Wananchi pia ndiyo Mabingwa watarajiwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara maana mpaka sasa hana mpinzani wakiwa na point 74 huku mshindani wake Simba akiwa na alama 67

Azam Sports Federation Cup mambo safi kwa #yangasc kwani wapo nusu fainali na watacheza na Singida Big Star wakishinda watawakabili @azamfcofficial mchezo wa Fainali.

Nabi akiwa na jeshi lake yupo Fainali Shirikisho Afrika, Ubingwa wa Ligi Kuu na Nusu Fainali ya FA ndani ya msimu mmoja.

Je ni wakati wa kujenga sanamu la Prof. Nabi akishinda mataji yote matatu.?

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents