Burudani

Je tutegemee Seduce Me Remix?, Man Water afunguka

Baada ya kuwepo version mbali mbali za ngoma Seduce Me ya Alikiba ikiwemo ile aliyofanya Man Water, producer huyo amefunguka juu ya version yake na iwapo itakuja remix.

Man Water kutoka studio za Combination Sound ilipofanyika ngoma hiyo, amesema version hiyo alifanya kutokana na ngoma hiyo kufanya vizuri ila huenda ikaja ikazaa remix.

“Siyo remix just flavor, ni kama cover katika version ya reggae na yenyewe imejitosheleza. Ni flavor kama appreciation ya namna ngoma ilivyosogea, unajua unaweza ukawa umekaa studio unajaribu kuchezea vitu tofauti tofauti ukawa umechokoza wazo kwa msanii au kwa watu wengine kusubiria jambo,” Man Water ameiambia Bongo5.

“Mara nyingi huwa nafanya hivyo, unaweza hata usimwambie msanii wazo ukalifanya kivitendo na watu wanasikiliza, unaona sasa hivi limeanza kutumika kwenye Fiesta wanafanya live, sasa ndio wazo limeshapenya hadi huko” amesema.

Hata hivyo ameongeza kuwa iwapo msanii husika ataona ngoma hiyo inahitaji remix inawezekana kufanyika katika version nyingine si lazima iwe reggae kutoka namna hiyo ilivyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents