Habari

Jerry Muro aomba Mh. Lema awe msemaji mpya wa Chadema

Aliyekuwa Msemaji wa klabu ya Yanga na mwandishi wa habari Jerry Murro amewaomba viongozi wa upinzani (Chadema) kumpa nafasi ya usema wa Chama hicho Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema kwa kuwa amekuwa akiongea zaidi kuliko wasemaji wa Chama hicho.

Muro akizungumza leo na waandishi wa habari amesema kuwa kuanzia leo hii kiongozi huyo anapaswa kuwa Msemaji mpya wa Chadema.

“Lema nikukumbushe wananchi wa Arusha wameingia mkataba na wewe wa wewe kuwaletea maendeleo na hio ndio kazi kubwa watu wa Arusha waliokupa, wananchi wa Arusha hawawakukutuma ukawe msemaji au Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chadema wananchi wa Arusha hawakukutuma ukapambane na Jerry Muro leo jimbo la Mhe. Lema halina hospitali na hospitali zilizopo ni za mashirika,” alisema Muro.

“Muulize Mbowe muulize Mashinji na muulize msemaji wa Chadema Lema, jamani naomba kuanzia Leo mimi nimuite Lema Msemaji wa Chadema na namuomba Mashinji na Mhe. Mbowe pamoja na cheo cha Ubunge embu muongezeeni Lema na cheo cha usemaji ili akapambane na wakina Polepole, embu muulize Msemaji wa Chadema bwana Lema mbona watu wanaotumia majina ya Chama chao kutukana watu mbona hawaendi polisi? Kama hawa watu hawatumwi na wao mi najua hawa wanatumwa na Chadema na leo niwaambie Watanzania angalieni watu wote wanaonitukana utaona wameweka kipicha cha Tundu Lissu Pray for Tundu Lissu, alisema Jerry.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents