Burudani

Jibu la Nikki wa Pili kwa Mhe. Nassari kuhusu Sugu

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Nikki wa Pili amejibu madai ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kuwa wasanii hawajaonyesha umoja kwa kile anachopitia msanii Sugu ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini.

Hapo awali Mhe. Nassari alisema wasanii wameshindwa kupaza sauti wakati huu ambao Sugu yupo mahabusu. Kupitia ukusara wake wa twitter ameandika.

Wasanii wa Bongo flava, mmesahau kabisa harakati za SUGU kupigania muziki wenu usimame? SUGU yupo mahabusu siku kumi, wasanii mmepiga kimya, court hamtokei, Jela hamfikii kumuona, mmeamua kumtumikia “kafiri?” Mmesahau alianzisha harakati za Kugoma kuimba bure?

Nikki wa Pili amejibu hilo kwa kusema, “wasanii hawana umoja, chama chao hakina nguvu kwa hiyo hata kunapotokea jambo wasanii walitolee sauti kwa pamoja kuna hakuna ‘platform’ ya kushikilia jambo hilo na kujikuta kila msanii yupo peke yake, na kupaza sauti kila mtu peke yake wasanii wengi wanaogopa hilo,” amesema.

Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anadaiwa kutoa maneno yenye kuleta chuki baina ya wananchi na serikali katika mkutano walioufanya December 30 mwaka jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents