Habari

Jinsi ya kuugeuza mwaka 2015 kuwa wenye mafanikio kikazi

Mchangiaji kwenye website ya Forbes.com, Lisa Quast amekuandalia mambo kadhaa ambayo ukiyazingatia unaweza kuugeuza mwaka 2015 kuwa wenye mafanikio kwako kazini.

We_Can_Do_It!

Jitame kwenye kioo

Anza kwa kujiona mwenyewe kama bidhaa yenye ushindani. Andika orodha ya nguvu zako, udhaifu na utofauti na kisha jipe changamoto mwenyewe kwa kukabiliana na udhaifu wowote na kujiboresha.

Fafanua mataminio yako ya kikazi

Kama hujui wapi unataka kwenda, utafikaje hapo? Chukua muda kufafanua ndoto zako. Unataka kuwa wapi kwenye kazi yako katika miaka mitatu, mitano, kumi ijayo?

Jitahidi ufahamu ushindani

Ushindani ni ukweli kuhusu maisha. Ujuzi wako unawazidi vipi wengine? Kuelewa ushindani wako kutakusaidia kutambua advantage na vitisho, na kukusaidia kuamua kuhusu hatua unazotakiwa kuchukua ili kushindana kwa kujiboresha mwenyewe.

Tambua malengo yako na tengeneza mpango wako

Malengo humulika kile unachotaka kufanikisha kujiboresha mwenyewe na kuendelea kusonga mbele kwenye kazi yako. Malengo yanakuhakikishia kuwa unaelekea kwenye uelekeo sahihi na utafikia ndoto zako haraka na kwa uhakika.

Usisubiri kuanza

Hakuna muda mwingine kama sasa. Usiache hofu ya usiyoyajua ikukwamishe. Mipango mikakati ya kazi, kama mawazo, hufanya kazi kama tu ukiitekeleza.

Sherehekea mafanikio yako

Usisubiri wengine wamulike mafanikio yako. Jipe moyo mwenyewe na zawadi (viatu vipya, kwenda movie au special dinner), kukusaidia kukupa motisha katika njia unayopitia kufikia ndoto zako za kazi.

Kama ule usemi wa zamani usemavyo: ‘Kama ukiendelea kufanya kile ulichozea kufanya, utaendelea kuwa pale ulipozea kuwa.’ Ufanye 2015 mwaka wa kubadilisha kile umekuwa ukifanya kwa kuthubutu kuota, na kisha kutengeneza mpango wa vitendo utakaokusaidia kufikia ndoto zako za kazi. Unaweza kufanya.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents