Michezo

Job awashusha presha Mashabiki Yanga

Beki wa Klabu ya Yanga Dickson Job leo katika mkutano na Waandishi wa Habari leo amewashusha mashabiki presha kuelekea mchezo wao wa Kesho dhidi ya CR Belouizdad ya Nchini Algeria, Wananchi kwa sasa malengo yao ni kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa kesho ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele kuelekea Robo Fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Dickson Job amesema ” kwa niaba ya wachezaji wenzangu tumejiandaa vizuri na mchezo wa kesho, mwanzo lengo letu lilikuwa ni kuingia hatua ya makundi baada ya muda merfu lakini kwa sasa lento letu kwa pamoja nib kupambana na kusonga mbele zaidi kwa kila mchezo uliokuwa mbele.”

Pia waandishi walimuuliza Job juu ya hali ya nyota mwenzie ambae siku ya mchezo  huo imepatiwa jina lake “PACOME DAY” alijibu ” Pacome hana Presha yoyote anajua umuhimu wa mchezo wa kesho na wachezaji wote tuko nyuma yake kumpa sapoti kwenye siku yake hii kubwa kama wachezaji wengine ambao wametangulia. Wote tutapewa mechi na hii ni heshima kubwa sana kwetu” Dickson Job akiwajibu waandishi wa habari.

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents