Michezo

Simba rekodi mbovu ASEC watamba

Kuelekea mchezo wa leo Klabu Bingwa Afrika Klabu ya Simba inakumbwa na wimbi la rekodi mbaya wakiwa ugenini simba mpaka sasa michezo yake mitano ya mwisho akiwa ugenini hajaambulia ushindi hata mchezo mmoja hii ikiwa ni ishara mbaya kwa mnyama akiwa ugenini huko Ivory Coast kwenye Uwanja wa Stade Felix Houphouet-Boigny akiwa anavaana na kinara wa kundi B akiwa amejiwekea kibindoni alama zake 10 huku Wekundu wa Msimbazi wakiwa na alama 5 tu.

Michezo 5 ambayo Simba amecheza akiwa ugenini;

Raja Casablanca ya Morocco dhidi ya Simba (3-1).

Wydad Casablanca ya Morocco dhidi ya Simba (1-0).

Power Dynamosya Zambia dhidi ya Simba (2-2).

Jwaneng Galaxy ya Botswana dhidi ya Simba (0-0).

Wydad Casablanca ya Morocco dhidi ya Simba (1-0).

 

Wakati huohuo wenyeji wao ASEC Mimosas akiwa na rekodi nzuri nyumbani kwake katika mechi 5 za mwisho kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

ASEC Mimosas dhidi ya USM Alger ya Algeria (0-0).

ASEC Mimosas dhidi ya Cotton Sport ya Cameroon (2-0).

ASEC Mimosas dhidi ya Ahly Benghazi ya Libya (2-1).

ASEC Mimosas dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco (1-0).

ASEC Mimosas dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botwasana (3-0).

Simba watakuwa na wakati mgumu katika mchezo huu hata rekodi zinawakataa kwa sasa ili kubakiza matumaini ya kuvuka robo fainali Simba anatakiwa asipoteze mchezo wa leo nafasi ya pili bado wote waliobaki kwenye kundi lao wanaweza kuifikia isipokuwa kinara wao tu ASEC Mimosas aliekwishajiwekea uhakika wa kwenda robo.

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents